Kuria amtaka Rais aunde kamati ya Bunge ili kuokoa mapendekezo muhimu ya BBI

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, sasa anamtaka Rais Uhuru Kenyatta kubuni kamati maalum ya Bunge ili kujadili namna ya kupitisha mapendekezo yenye manufaa katika mpango wa BBI.

Kuria amesema hatua hiyo itasaidia kuepusha hali ya mpango huo kutupiliwa mbali kwa kukosa uungwaji mkono.

Kuria amedumisha kwamba nchi hii haistahili kupoteza mapendekezo kadhaa muhimu katika mpango wa BBI, kama vile kuongezwa kwa kiwango cha fedha zinazotolewa kwa kaunti na kubuniwa kwa maeneo bunge mapya kwenye kaunti ambako hakuna uwakilishi wa kutosha.

Also Read
Wazee watakiwa kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ukabila nchini

Amekariri kwamba juhudi za kuandaa kura ya maamuzi kuambatana na hali ilivyo sasa humu nchini zitasababisha BBI kukosa uungwaji mkono wa kutosha kote nchini.

Also Read
Ruto na wafuasi wake wataka kura ya maamuzi ya BBI ifanyike 2022

Akiongea katika eneo la Gatundu Kaskazini baada ya hafla ya mazishi katika Kijiji cha┬áKang’oo, Kuria ametoa wito kwa kiongozi wa taifa kuandaa mkutano wa kundi la wabunge wa vyama mbali mbali ili kujadili uwezekano wa kupitisha bungeni mapendekezo muhimu kwenye ripoti hiyo ya BBI.

Also Read
Mwezi Julai ndio utakaokuwa kilele cha msimu wa baridi

Amesema ijapo ripoti hiyo ni nzuri, taratibu zinazohitajika kabla ya kufanyia katiba marekebisho hazijafuatwa.

Aidha, Kuria amesema inasikitisha kuona kwamba kutokana na tamaa za kibinafsi, baadhi ya wanasiasa wametumia ripoti ya BBI kama chombo cha kuzua ghadhabu miongoni mwa Wakenya wengi.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi