Kutakuwa na maziwa ya bure siku ya kusherehekea kupandishwa hadhi kwa mji wa Nakuru

Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika kaunti ya Nakuru wameahidi kutoa maziwa bila malipo wakati wa sherehe zinazotarajiwa kuandaliwa kusherehekea hatua ya hivi maajuzi ya mji huo kupandishwa hadhi  na kufanywa kuwa jiji.

Afisa wa kamati kuu ya kaunti hiyo anayehusika na maswala ya kilimo Dkt. Immaculate Maina amesema kuwa uamuzi huo una kumbukumbu kadhaa za kihistoria.

Also Read
Serikali ya Kaunti ya Nakuru yashirikiana na Uingereza kuimarisha mauzo ya mboga na maua

Afisa huyo anasema kuwa mji huo ulianzishwa na wafugaji wa ngombe wa maziwa wa kikoloni ambao walianzisha kampuni ya utayarishaji maziwa ya KCC, ambayo imekuwa ikitayarisha maziwa humu nchini tangu taifa hili kujipatia uhuru.

Also Read
Watu 7 zaidi wafariki kutokana na makali ya Covid-19 hapa nchini

Mwenyekiti wa chama cha wafugaji hao Waweru Nyangi amesema kuwa wafugaji hao wanahisi kuwa wanapaswa kuonyesha shukrani kwa serikali ya kaunti hiyo kuhusiana na namna ambayo imekuwa ikiwathamini.

Also Read
Waumini wa Kisii walalamikia ongezeko la visa vya makanisa kuteketezwa

Waweru alisema kuwa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa bado una faida kubwa zaidi katika kaunti hiyo kutokana na mazingira bora na kuwepo kwa vyama bora vya ushirika ambavyo vimefanikisha uuzaji wa maziwa hayo.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi