Kutoonekana kwa Rais Magufuli hadharani kwaibua wasiwasi Tanzania

Wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, wameibua wasi wasi kuhusu afya ya Rais John Pombe Magufuli, ambaye hajaonekana hadharani kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Kwa miezi kadhaa, Magufuli mwenye umri wa miaka 61-alisisitiza kwamba ugonjwa wa COVID-19 umetokomezwa kwa njia ya maombi, huku akipuuza hatua muhimu kama vile utumizi wa barakoa na kufungwa kwa shughuli za kiuchumi.

Also Read
Ushirikiano kati ya nchi kubwa na Afrika unatakiwa kuinufaisha Afrika na sio kuwa uwanja wa mivutano

Hata hivyo mwezi uliopita alikiri kwamba ugonjwa huo ulikuwa bado ukisambaa kufuatia dokezi kwamba Makamu wa Rais wa Zanzibar alifariki kutokana na virusi vya Corona.

Mara ya mwisho Magufuli kuonekana hadharani ilikuwa tarehe 27 wezi jana wakati wa hafla ya kuapishwa kwa afisa mmoja wa serikali katika Ikulu ya Dar-es-Salaam.

Also Read
Ba N'Daou ateuliwa kaimu Rais wa Mali

Kufikia sasa serikali ya Tanzania haijabainisha mahali aliko Rais huyo, Ijapo siku ya Jumatano, waziri wa habari nchini humo Innocent Bashungwa aliwatahadharisha waandishi wa habari na pia raia dhidi ya kueneza uvumi kuhusu rais huyo.

Also Read
Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tanzania iliacha kuchapisha takwimu kuhusu janga la Corona mwezi April 2020, mnamo mwezi Januari mwaka huu.

Magufuli alisema kuwa chanjo za kupambana na ugonjwa wa Covid-19 ni hatari.

  

Latest posts

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdock wakamatwa na kupelekwa mafichoni

Dismas Otuke

Vikosi vya usalama vyazima jaribio la mapinduzi nchini Sudan

Tom Mathinji

China yaadhimisha miaka 50 tangu kurudishiwa kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi