KWS yatenga shilingi milioni 17 kuwafidia waliojeruhiwa na wanyama pori Kajiado

Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori Nchini (KWS) limetoa shilingi milioni 17 kama fidia kwa wahasiriwa waliovamiwa na wanyama wa porini katika Kaunti ya Kajiado.

Hatua hii ni afueni kwa wahasiriwa hao baada ya subira ya muda mrefu, wakati ambapo kumeshuhudiwa mzozo kati ya binadamu na wanyama kwenye njia ya uhamiaji ya wanyama hao.

Waziri wa Utalii na Wanyama Pori Najib Balala amethibitisha kwamba wizara yake imetoa kima hicho cha shilingi milioni 17 zitakazopewa wahasiriwa hao katika muda wa wiki mbili zijazo.

Also Read
Raila aahidi ukombozi wa wanawake kupitia BBI

Balala amesema kuwa serikali inafanya juhudi za kupunguza mizozo kati ya binadamu na wanyama ili kuzuia visa vya wanyama kuuawa na wakazi wenye gadhabu katika eneo linalopakana na Mbuga ya Kitaifa ya Amboseli.

Wakazi wa eneo hilo wameitaka serikali kuharakisha utoaji wa fidia hizo, huku wakishtumu KWS kwa kulemaza mchakato wa ulipaji wa fidia hizo licha ya baadhi yao kujeruhiwa vibaya na wanyama.

Also Read
Eneo la kiuchumi kujengwa katika kaunti ya Kisumu

Gavana wa Kaunti hiyo ya Kajiado Joseph Lenku pia ameshinikiza kufidiwa kwa wahasiriwa wote kwa pamoja.

Kaunti Ndogo za Kajiado Kusini, Mashariki na Magharibi ndizo zilizoshuhudia visa vingi zaidi vya mzozo kati ya binadamu na wanyama.

Also Read
Kenya yanakili visa 536 zaidi vya Covid-19

Mwaka wa 2019, watu watatu waliuawa na ndovu katika Kaunti Ndogo ya Mashuru.

Kulingana na takwimu kutoka kwa shirika la KWS, jumla ya watu 23 wameuwa na wanyama pori katika kaunti hiyo tangu mwaka wa 2012.

Aidha, zaidi ya watu 134 wamejeruhiwa vibaya na wanyama hao, mifugo wapatao 1,000 kuuawa na mali yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 kuharibiwa.

  

Latest posts

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Visa 323 vipya vya COVID-19 vyathibitishwa hapa nchini

Tom Mathinji

Ujenzi wa reli kati ya Mai Mahiu na Longonot wakamilika

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi