Lewandowski Aonyesha Nia ya Kugura Bayern Munich

Mshambulizi Robert Lewandowski amekiambia kilabu cha Bayern Munich kuwa anataka kukiaga mwisho wa msimu huu.

Mshambulizi huyo wa umri wa miaka 33 amefunga mabao 343 katika mechi 373, na ni mfungaji bora wa pili kwenye kilabu hicho nyuma ya Gerd Muller tangu alipowasili mwaka 2014.

Also Read
Kipute cha Yuro kuanza kutimua vumbi Ijumaa

Lewandowski, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu ujao, amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Barcelona.

Also Read
Liverpool na Ajax zatinga raundi ya 16 bora ligi ya mabingwa ulaya

Tangu alipotoka Borussia Dortmund, Lewandowski ametwaa taji ya ligi kuu katika misimu yake yote minane na alitwaa taji ya ligi ya kilabu bingwa barani Ulaya msimu wa mwaka 2019-20.

Also Read
Bayern Munich watwaa kombe la dunia baada ya kuwazidia maarifa Tigres

Mwaka jana, Lewandowski alivunja rekodi ya Muller ya miaka 49 ya kufunga mabao mengi ya Bundesliga katika mwaka mmoja alipofunga mabao 43 katika mechi 34.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi