Ligi kuu FKF kuingia raundi ya 15 Wikendi Ingwe wakiwa na miadi na Sharks

AFC leoapards watashuka uwanjani Kasarani Jumamosi hii kuanzia saa tisa Alasiri kumenyana na Kariobangi Sharks ,kwa mechi ya ligi ikiwa raundi ya 15.

Ingwe watawinda kusajili ushindi ili kujikwamua kutoka eneo la kushushwa daraja wakiwa na alama 14 kutokana na mechi 13 ,nao Kariobangi Sharks walio katika nafasi ya 9 kwa alama 21.

Also Read
Wycliffe Ogalo atimuliwa wadhifa wa Kamishna Mkuu wa magereza nchini

Katika mipambano mingine ya wikendi hii Kenya Commercial Bank itakuwa Utalii grounds dhidi ya Kakamega Homeboyz pia saa tisa ,wakati maafande wa Kenya Police wakipimana nguvu na Mathare United katika kiwara cha Kasarani.

Jumapili Wazito FC wanaokabiliwa na matatizo ya kifedha watakuwa Nyayo Stadium kuwajulia hali Nzoia Sugar inayowania ushindi wa pili wa msimu,nazo Sofapaka na Bidco United zitakuwa uwanja wa manispaa ya Thika saa tisa Alasiri ,Vihiga Bullets watakuwa nyumbani Bukhungu dhidi ya Bandari FC .

Also Read
AFC Leopards wazindua uzi mpya wa nyumbani

Mabingwa watetzi Tusker watakuwa nyumbani Ruaraka dhidi ya Nairobi City Stars Jumapili saa tisa ,wakilenga kujizoa baada ya kupigwa na Posta Rangers wiki jana.

Also Read
FKF yalalama kuhusu kukosekana kwa viwanja nchini

Gor Mahia watativua kivumbi dhidi ya Talanta Jumapili hii nao Posta Rangers wamalize udhia na Ulinzi Stars ugani Thika Municipal.
THIKA STADIUM, THIKA

  

Latest posts

Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Marion Bosire

Didmus Barasa Ajisalimisha kwa Maafisa wa Polisi

Marion Bosire

Chebukati: Tutaharakisha zoezi la kujumlisha matokeo ya kura za Urais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi