Serikali ya Rwanda imefutulia mbali mechi za ligi kuu nchini Rwanda baada ya wasimamizi na timu kukosa kuzingatia masharti yote ya Covid 19 yanayohitajika.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya Habari Shirikisho la soka nchini humo Ferwafa limesikitishwa na hatua hiyo ya serikali lakini limeahidi kuzingatia masharti yote dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 kuhakikisha ligi hiyo inarejelewa haraka iwezekanavyo.
Mechi tatu za ligi hiyo msimu huu zilikuwa zimechezwa kabla ya kusimamishwa .
Marines wanaongoza jedwali baada ya michuao mitatu kwa pointi 7 wakifuatwa na musanze walio na alama 1.
Hata hivyo serikali ya Rwanda imesisitiza kuwa michuano ya kombe la Cecafa kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17 inayoanza Jumapili itaendelea ilivyopangwa baada ya waandalizi kuzingatia masharti yanayohitajika.