Ligi kuu ya Kenya KPL kuendelea Jumatano kwa mikwangurano minne

Ligi kuu ya kandanda nchini Kenya,KPL,itaendelea Jumatano April 6 huku jumla ya mechi nne zikisakatwa katika nyuga mbalimbali.

Mathare United wanaokabiliwa na hatari ya kuenguliwa ligini watakuwa nyumbani dhidi ya Vihiga Bullets,mchuano ambao vijana wa Mathare hawana budi kushinda , ili kufufua  matumaini ya kusalia ligini huku pia Bullets wakiwania ushindi ili kuimarisha matumaini ya kuepuka shoka.

Also Read
Wafalme wa kutoka sare Ulinzi Stars wasajili sare ya nne ligini dhidi ya Bidco United

Katika mechi nyingine Kakamega Homeboyz wanaowinda ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya kwanza,  watakuwa katika kaunti ya Taita Taveta uwanja wa Wundanyi kumenyana na Sofapaka,nao AFC Leopards ambao wameimarika pakubwa wakiwa wageni wa Wazito Fc.

Also Read
Zimbabwe kuweka kando masaibu ya COVID 19

Bidco United watapimana nguvu na Posta Rangers katika pambano jingine la katikati ya wiki.

Homeboyz wangali kileleni kwa alama 52  kutokana na mechi 24,pointi 10 zaidi ya mabingwa watetezi Tusker Fc huku  Nairobi City Stars na Gor Mahia zikishikilia nafasi za 3 na nne mtawalia kwa alama 41 kila moja.

Also Read
Waziri Amina avunja FKF na kubuni kamati

Mathare United ni ya mwisho ligini kwa alama 11,nyuma ya Vihiga iliyo na alama 16  nayo Wazito FC ni ya 16 kwa pointi 20.

  

Latest posts

IEBC kutangaza rasmi matokeo ya Urais Jumatatu

Dismas Otuke

Andrew Mwadime ndiye Gavana mpya wa Taita Taveta

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 12 zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi