Ligi kuu ya Kenya kurejea kwa mechi za raundi ya pili

Ligi kuu ya Kenya itarejea Ijumaa kwa michuano ya raundi ya pili baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
Bandari FC walioshinda mechi ya ufunzguzi dhidi ya Mathare United watakuwa katika uchanjaa wa manispaa wa Thika kuanzia saa saba mchana dhidi ya Bidco United waliosajili sare katika mchuano wa ufunguzi.

Also Read
Peres Jepchirchir na Brigid Kosgei wanyakua dhahabu na fedha ya marathonpe

Baadae saa tisa na robo alasiri Posta Rangers watakabana koo na Vihiga Bullets iliyopandishwa ngazi msimu huu ,mechi pia ikisakatwa uwanjani Thika Municipal.

Also Read
Kocha mpya wa Harambee Stars Engin Firat kutoka Uturuki kuzinduliwa Jumapili

Batoto Ba Mungu Sofapaka wako ziarani saa tisa alasiri katika uwanja wa Sudi kaunti ya Bungoma dhidi ya Nzoia Sugar.

Mechi zaidi za ligi hiyo kupigwa Jumamosi,KCB wakipimbana ubabe na AFC Leopards,Mathare united iwaalike Ulinzi Stars,Police FC iwaalike Nairobi City Stars huku Wazito Fc ikiwa na miadi dhidi ya Kakamega Homeboyz.

Also Read
KBC Channel 1 kupeperusha mechi ya Kenya dhidi ya Zambia Ijumaa

Msimu wa ligi kuu mwaka 2021-2022 ulianza Septemba 25 kwa mechi za mzunguko wa kwanza.

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi