Kulingana na Fkf ligi hiyo imesukumwa mbele kwa wiki moja kutoka tarehe ya awali, baada ya ligi kuu ya FKF kuahirishwa kutoka Novemba 20 hadi Novemba 27.
Ligi ya NSL itashirikisha timu 17 msimu huu kinyume na 19 za msimu jana baada ya Chemilil Sugar Fc na Ushuru Fc kuvunjiliwa mbali kutokana na ukosefu wa pesa na hivyo basi kutoa fursa kwa Silibwet Leos Fc,Soy United na Mwatate United Fc kupandishwa ngazi kucheza ligi hiyo.
Timu mbili bora kutoka ligi hiyo hupandishwa ngazi kucheza ligi kuu ya FKF huku ile ya tatu ikicheza mchujo dhidi ya timu ya 16 katika ligi kuu ambapo mshindi hushiriki ligi kuu.
Wachezaji wa vilabu vyote vya ligi kuu wanapitia vipimo vya Covid 19 kwa mjibu wa matakwa ya serikali kabla ya ligi kuanza rasmi.
Ligi kuuu ya Fkf msimu wa mwaka 2020-2021 uantazamiwa kuanza mwishoni mwa juma hili kwa mechi tatu Afc Leopards wakipambana na Posta Rangers katika uwanja wa Nyay,o huku Mathare united ikifungua dimba dhidi ya Kakamega Homeboyz nao Bandari Fc waanze msimu nyumbanio dhidi ya Zoo Fc.