Linturi ashtakiwa kwa jaribio la ubakaji

Seneta wa Meru Mithika Linturi amefunguliwa mashtaka ya jaribio la ubakaji kwenye mahakama moja hapa Nairobi.

Linturi pia anakabiliwa na shtaka la pili la kumpapasa mlalamishi.Seneta huyo pia anakabiliwa na shtaka la kujaribu kumbaka mwanamke mmoja wa umri wa miaka 36 kwenye hoteli ya Mayani Villa huko Nanyuki, kaunti ya Laikipia .

Also Read
Polisi wamewaua washukiwa watano wa ujambazi Jijini Mombasa

Hatahivyo, Linturi aliyefikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Martha Nazushi alikanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa thamana ya shilingi elf 200 pesa taslimu.

Also Read
Mbunge wa zamani wa Laikipia mashariki ashtakiwa kwa wizi wa ardhi

Mawakili wa Linturi wakiongozwa na Mothomi Thiankolu walikuwa wameiomba mahakama imuachilie kwa thamana.

Upande wa mashtaka ukiongozwa wakili Evelyne Onunga awali ulikuwa umeiambia mahakama kuwa Linturi alitekeleza makosa hayo tarehe 30 mwezi Januari mwaka huu.

Also Read
Serikali za Kaunti zahimizwa kukumbatia utalii wa maonyesho ya kitamaduni

Jaribio kla mshtakiwa la kutaka kuzuyia mashtaka hayo katika mahakama kuu mwezi jana liligonga mwamba.Kesi hiyo itatajwa tarehe 26 mwezi oktoba mwaka huu.

  

Latest posts

Aliyekuwa mtangazaji Mwanaisha Chidzuga ajitosa katika ulingo wa siasa

Tom Mathinji

#KisaChangu: Dr Mukhisa Kituyi kuwania urais ili kukamilisha safari ya ukombozi

John Madanji

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi