LSK yapinga vikali kuapishwa kwa Kananu kuwa Naibu Gavana wa Nairobi

Chama cha Wanasheria humu nchini (LSK) kimesema kitawasilisha kesi mahakamani kupinga hatua ya kuapishwa kwa Anne Kananu Mwenda kuwa Naibu Gavana wa Kaunti ya Nairobi.

Rais wa chama hicho Nelson Havi ametaja hatua ya kuapishwa kwa Kananu kuwa mapinduzi dhidi ya katiba ya taifa hili.

Also Read
Jiji la Nairobi kukumbwa na uhaba wa maji kwa siku mbili kuanzia Alhamisi

Haraka iliyokuwepo katika kusailiwa kwa Kananu, kuidhinishwa kwake na Bunge la Kaunti ya Nairobi na hatimaye kuapishwa siku ya Ijumaa, imeibua maoni tofauti miongoni mwa Wakenya, vyama vya kisiasa, wanaharakati na pia mawakili, huko wengi wakitilia shaka uhalali wa utaratibu huo.

Also Read
Watu 184 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kuapishwa kwake kuwa Naibu Gavana wa kwanza mwanamke katika Kaunti ya Nairobi huenda kukasababisha kuwasilishwa kwa kesi mbali mbali mahakamani kuanzia Jumatatu.

Also Read
Shirika la Ndege nchini larejelea safari za ndege katika kaunti tano zilizokuwa zimefungwa

Chama cha Thirdway Alliance Kenya, ambacho tayari kimewasilisha kesi mahakamani dhidi ya Kananu, kimeshtumu utaratibu huo na kuutaja kuwa haramu na ishara wazi ya kutotiliwa maanani kwa  utawala wa sheria.

  

Latest posts

Jimmy Wanjigi afikishwa Mahakamani

Tom Mathinji

Wataalam wa uchunguzi wapelekwa katika mto Yala

Tom Mathinji

Mwanafunzi akufa maji katika bwawa kaunti ya Kitui

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi