Lulu ajifungua

Muigizaji wa filamu za Bongo nchini Tanzania Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amejifungua mtoto wa kiume.

Habari hizo zimetolewa na mume wake Francis Ciza kupitia mitandao ya kijamii.

Mmiliki huyo wa kituo cha redio cha E Fm na kituo cha runinga cha Tv E ambaye anajiita Majizzo kwenye mitandao ya kijamii alipachika picha yake akiwa na mke wake mjamzito kwenye Instagram akisema wamejaliwa mtoto wa kiume kwa jina G.

Also Read
Ommy Dimpoz kujiunga na Sony Music Africa

Kulingana naye, wamekuwa wakiitana Baba G na Mama G kwa muda mrefu huku wakijitia imani lakini sasa ombi lao limejibiwa na G amewasili duniani.

Majizzo aliongeza kusema kwamba mama na mtoto wako salama salimini. Watu wengi maarufu nchini Tanzania wamepongeza wanandoa hao kwa kujaliwa mtoto wakiwemo Babu Tale ambaye ni mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na meneja wa Diamond Platnumz, Muigizaji Aunt Ezekiel, wanamuziki Barnaba Classic na Rosa Ree na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo.

Also Read
Akon aingilia biashara ya madini nchini Congo

Baada ya kuchumbiana rasmi mwezi Oktoba mwaka 2018, wawili hao Lulu na Majizzo walifunga ndoa tarehe 16 mwezi Februari mwaka huu wa 2021.

Harusi yao ilihudhuriwa na watu wachache ambao wengi wao walikuwa wa familia.

Alipohojiwa Majizzo alisema aliamua kufanya arusi ya gharama ndogo ili kuonyesha vijana kwamba wanaweza kufanya harusi hata bila fedha nyingi.

Also Read
Rais mcheshi azindua kitabu

Kitu ambacho alisema kilikuwa ghali ni mavazi yao ya harusi.

Hata hivyo Mange Kimambi ambaye ni mwanaharakati mzaliwa wa Tanzania anayeishi Marekani alipachika ujumbe aliotumiwa na mtu ambaye hakumtaja ambao unaonyesha kwamba wakati wa harusi Majizzo alitumia shilingi milioni moja pesa za Tanzania kukodi chumba cha hoteli ambacho Lulu alikuwa akitumia.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi