Maafisa 35 wa KRA washtakiwa kwa madai ya ufisadi

Maafisa 35 wa Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru nchini, KRA, wameshtakiwa kwa mashtaka mbalimbali ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka.

Kati ya  35 hao, maafisa watano hawakufika mahakamani kutokana na sababu mbalimbali.

Maafisa hao walishtakiwa kwa madai mbali mbali likiwemo kusaidia kampuni mbali mbali kukwepa kulipa ushuru kati ya mwezi Novemba 2019 na Aprili 2019.

Also Read
Mwilu ataka vikao vya mahakama virejelewe kikamilifu

Wale waliofika mahakamani walikanusha mashtaka dhidi yao na kuachiliwa kila mmoja kwa dhamana ya shilingi laki mbili au bondi ya shilingi milioni moja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Also Read
Wahudumu wa matatu Nakuru watishia kurejea mjini

Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani ya kupambana na ufisadi Douglas Ogoti aliwaagiza wale waliokosa kufika mahakamani kupewa hati za kuwataka kufika mahakamani.

Washukiwa wanahitajika kusalimisha pasipoti zao, huku wale wasio na pasipoti wakizuiliwa kuondoka katika eneo la mahakama.

Washukiwa walizuiliwa kuzuru afisi za KRA, iwapo hawataandamana na afisa wa uchunguzi.

Also Read
Ndindi Nyoro apigwa marufuku kuhudhuria vikao vya bunge

Vikao vya kwanza vya Kesi hiyo vinatarajiwa kuandaliwa tarehe mosi mwezi Disemba mwaka huu.

Washukiwa hao walishtakiwa baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali ombi lao la kutaka kuzuia kushtakiwa kwao siku ya Ijumaa.

 

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi