Maafisa wa idara ya mahakama waonywa dhidi ya utepetevu kazini

Kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu amewatahadharisha maafisa wa idara ya mahakama dhidi ya kuchelewesha haki akisema hatua kali itachukuliwa wale watakaopatikana wakitatiza shughuli za mahakama.

Mwilu amesema maafisa wa idara ya mahakama wanafaa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kufanikisha juhudi za kutafuta haki bila kukubali kushawishiwa na mtu yeyote.

Also Read
Visa 1,506 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Akiongea wakati wa ufunguzi wa sajili ndogo ya mahakama kuu na mahakama ya kushughulikia kesi za mazingira na pia mahakama ya kushughulikia kesi za ardhi katika mahakama ya Kilgoris Trans Mara Magharibi kaunti ya  Narok, Mwilu alisema vitendo vya maafisa wa idara ya mahakama vinafaa kuwa vya uadilifu mkubwa.

Also Read
Kalonzo akosoa uamuzi wa Mahakama Kuu wa ‘kumsimamisha kazi’ Kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu

Alisema ufunguzi huo wa sajili ndogo ya  mahakama ya mazingira na mahakama ya ardhi katika eneo hilo unatarajiwa kuboresha jinsi ya kushughulikia kesi za ardhi ambazo zimekuwa zikisababisha taharuki isiyofaa miongoni mwa wakazi.

Viongozi wa eneo hilo wametoa wito kwa Mwilu kuhakikisha mahakama hazitumiwi na polisi na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kutatua masuala ya  kisiasa.

Also Read
Kesi dhidi ya kiongozi wa zamani wa PCEA David Gathanju yaahirishwa

Huku mimba na ndoa za mapema zikiwa zimekithiri katika kaunti ya Narok, gavana Samuel Tunai alitoa wito kwa kaimu jaji mkuu kupeleka maafisa zaidi wa idara ya mahakama katika eneo hilo ili kushughulikia kesi hizo.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi