Maafisa wa KDF wamuua mwanamgambo wa Alshabab kaunti ya Lamu

Vikosi vya ulinzi vya Kenya (KDF) vinavyohudumu katika msitu wa Boni chini ya oparesheni ‘Amani Boni’, viliwafumania na kusambaratisha Kundi moja la wanamgambo wa Alshabab katika barabara ya Milimani-Baure eneo la  Malindi, kaunti ya Lamu.

Also Read
Mike Mbuvi Sonko atimuliwa mamlakani

Kulingana na taarifa,  katika tukio hilo la Jumatano asubuhi, mwanamgambo mmoja wa Alshabab aliuawa huku wengine kadhaa wakitoroka wakiwa na majeraha ya risasi.

Also Read
Raila amzomea Mutunga kutokana na barua aliyomwandikia Rais

Wanajeshi hao walipata bunduki moja aina ya AK47, huku wakiendelea kuwasaka wanamgambo waliotoroka.

Hakuna majeruhi yaliyoripotiwa Kwa wanajeshi wa KDF wakati wa makabiliano hayo.

Also Read
COVID-19: Serikali ya Kaunti ya Kilifi yapiga marufuku michezo

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, vikosi vya KDF pamoja na asasi zingine za usalama chini ya oparesheni ‘Amani Boni’, zimejitolea kukabiliana na vilivyo na magaidi wa Al-Shabaab.

  

Latest posts

Japhet Koome ateuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi

Tom Mathinji

Majukumu ya Naibu Rais Rigathi Gachagua yabainishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi ateuliwa waziri mwenye Mamlaka zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi