Maafisa wa Polisi kufaidika na Bima ya Matibabu iliyoboreshwa kuanzia Januari

Maafisa wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi na wale kutoka Idara ya Magereza nchini watafaidika na mpango wa bima ya maisha ulioboreshwa kuanzia mwezi Januari mwaka wa 2021.

Hii ni baada ya idara hizo kutia saini kandarasi na Shirika la Bima ya Kitaifa ya Afya (NHIF) kuhusu utoaji wa huduma hizo.

Makubaliano hayo yamejiri baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya wadau wa idara hizo na NHIF kwa lengo la kumaliza mizozo ya ulipaji wa fedha za bima kwa wanachama.

Also Read
Biashara zanoga Jomvu kufuatia kupungua kwa visa vya uhalifu

Katibu Mkuu wa Wizara Usalama Dkt. Karanja Kibicho amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali kuu za kuimarisha mpango wa kuwalinda zaidi ya maafisa 131,000 wa polisi wanaolazimika kukabiliana na mabadiliko ya kimaisha kila wakati.

“Kumekuwa na mabadiliko kadhaa katika kuwapa maafisa wetu huduma hizi na ndiyo sababu tuliamua kushirikiana na NHIF ili kuwalinda kama watumishi wengine wa umma,” amesema Kibicho baada ya kutia saini makubaliano hayo katika Jumba la Harambee.

Also Read
NHIF yatakiwa kutoa bima ya matibabu kwa aina zote za magonjwa ya saratani

Kulingana na Katibu huyo, lengo la mpango huo ni kuainisha utoaji wa bima kwa maafisa hao na watumishi wengine wa umma ili kuangazia matatizo ya familia za maafisa wanaopoteza maisha yao wakiwa kazini.

Also Read
Polisi wamkamata mmiliki wa shamba la bangi katika eneo la Soy

Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai ameusifu mpango huo, akisema utawapa motisha maafisa hao, kauli iliyoungwa mkono na Kamishna Jenerali wa Idara ya Magereza Wycliffe Ogallo.

Afisa Mkuu Mtendaji wa NHIF Dkt. Peter Gathege pia amesisitiza umuhimu wa mpango huo na akaahidi kuhakikisha kwamba malipo ya bima kwa maafisa hao yatakuwa yanatolewa kwa muda ufaao.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi