Maafisa wa Polisi kuwasimamia askari wa jiji la Nairobi

Halmashauri ya huduma za jiji la Nairobi NMS, pamoja na serikali ya kaunti ya Nairobi,zimemteua kamanda mmoja kutoka huduma ya taifa ya polisi kuwasimamia askari wa serikali ya jiji la Nairobi.

Katika mahojiano na runinga ya shirika la utangazaji nchini KBC, mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Nairobi Mohamed Badi, alisema wamewiainisha oparesheni za askari wa kaunti ya jiji la Nairobi almaarufu Kanjos kuwa chini ya uongozi mmoja.

Also Read
Serikali yajizatiti kukabiliana na visa vya moto Gikomba

“Askari wa jiji almaarufu Kanjos hawatoki katika vikosi vya usalama, kwa hivyo tunajaribu kuleta nidhamu kwa kuwaleta maafisa wa polisi wa cheo cha inspekta kuhakikisha nidhamu inadumishwa,” alisema Badi.

Badi alidokeza kuwa halmashauri ya NMS imeweka mikakati ya kutoa mafunzo upya kwa askari wa jiji la Nairobi katika chuo cha mafunzo kwa maafisa wa polisi  wa utawala ili kuboresha ujuzi wao.

Also Read
Maskwota wa Kilifi kupewa makazi na Serikali

Mkurugenzi huyo wa NMS alisema uhusiano mwema uliopo na serikali ya kaunti ya Nairobi, umesababisha mazingira mazuri kwa shirika la NMS kutekeleza majukumu yake ambayo ni pamoja na Uchukuzi,Afya,Nyumba, mazingira na huduma za maji.

Kwa mujibu wa Badi, NMS itakamilisha ujenzi wa hospitali 27 kabla ya kukamilika kwa mwezi July huku akidokeza kuwa tayari hospitali 6 zimezinduliwa na zingine 12 zikikaribia kuzinduliwa kufikia mwezi ujao.

Also Read
Halmashauri ya Usimamizi wa Jiji la Nairobi yapima wakaazi Korona

Kuhusu swala la afya, Badi alisema wahudumu 2,500 wa afya wameajiriwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora  za afya huku wauguzi na madaktari wakiwekwa katika mpango wa kitaifa wa bima ya afya NHIF.

Alisema walishirikiana na wawakilishi wadi kutambua miradi ya maendeleo iliyohitaji kipaumbele katika wadi zote Jijini Nairobi.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi