Maafisa wa polisi na wale wa NTSA wazindua msako dhidi ya wanaokiuka sheria za trafiki Bungoma

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Bungoma wameanzisha msako dhidi ya piki piki, tuk tuk na wahudumu wa uchukuzi wa umma ambao wanakiuka sheria za trafiki.

Akiwautubia wanahabari katika soko la Sikata katika barabara kuu ya Webuye-Malaba, kamishna wa kaunti ya Bungoma Samuel Kimiti aliyewaongoza maafisa hao wakati wa uzinduzi wa msako huo utakaochukua siku 30, alisema magari yote mabovu yatanaswa huku wahudumu wa boda boda wanaohudumu bila vifaa vinavyohitajika wakitiwa mbaroni.

Also Read
Sharlet Mariam ajitoa kwenye uchaguzi mdogo wa Msambweni

“Shughuli hii itaendeshwa katika kaunti  nzima ya Bungoma, kuhakikisha usalama wa wanaotumia barabara za humu nchini,” alisema Kimiti.

Maafisa wa polisi na wale wa NTSA watekeleza msako dhidi ya utundu barabarani katika kaunti ya Bungoma. Picha na KNA

Kulingana na Kimiti, msako huo unawalenga wahudumu wa boda boda, tuk tuk na madereva wa magari ya uchukuzi wa umma wanaokiuka sheria za barabarani.

Also Read
Wanaovuruga miundo msingi eneo la Pwani waonywa vikali

“Tumezindua zoezi hili katika barabara kuu ya Webuye-Malaba na lengo letu ni madereva wanaovunja sheria za trafiki,” alifoka Kimiti.

“Katika muda wa miezi mitatu iliyopita, taifa hili limewapoteza watu wengi kupitia ajali za barabarani, na ndio maana serikali imechukua hatua ya msako huu,” aliongeza kamishna huyo wa Bungoma.

Also Read
NTSA: Usalama barabarani kujumuishwa katika mtaala wa elimu

Mtawala huyo alitoa wito wa halmashauri ya usalama barabarani NTSA, kuhakikisha wahudumu wa boda boda ambao husababisha nyingi ya ajali za barabarani, wanafuatilia kikamilifu sheria za barabarani na wanaokiuka watiwe mbaroni.

  

Latest posts

Japhet Koome ateuliwa Inspekta Jenerali wa Polisi

Tom Mathinji

Majukumu ya Naibu Rais Rigathi Gachagua yabainishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi ateuliwa waziri mwenye Mamlaka zaidi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi