Maafisa wa Polisi Waongoza Matembezi ya Kuhimiza Amani Marigat

Maafisa wa polisi mjini Marigat wakiongozwa na Ocs Bwana Maalim Abdullahi, wameongoza wakazi wa mji huo na waumini wa makanisa mbali mbali mjini huko kwa matembezi ya kuhimiza amani uchaguzi mkuu unapokaribia. Akizungumza na mwanahabari wetu, Maalim alielezea kwamba waliaandaa matembezi hayo baada ya ibada kunako saa tano asubuhi ili kuhimiza wenyeji kupiga kura kwa amani. “Tuliungana na ACK Church na Town Fellowship Church ya Marigat na tukaongea tudumishe amani, tuhamasishe wananchi kwamba wakati huu wa election tudumishe amani.” alisema Maalim.

Also Read
Majaji wa Mahakama ya Rufaa watakiwa kuhudumu kwa uadilifu

Msimamizi huyo wa kituo cha polisi cha Marigat alisema kwamba matembezi hayo yalichochewa na visa ambavyo vimeshuhudiwa kwenye chaguzi za awali. Alisema kwamba kila mara uchaguzi unapowadia wananchi hujawa hofu wakidhania kwamba kutatokea machafuko na dhamira nyingine ya matembezi hayo ni kuhakikishia wananchi usalama.

Also Read
IEBC yasitisha shughuli ya kuhesabu kura za Kiambaa kufuatia malalamishi ya Jubilee

Washiriki wa matembezi hayo walizunguka mji wa Marigat huku wasimamizi wa uchaguzi katika eneo bunge la Baringo Kusini ambapo mji huo uko wakiendeleza juhudi za kugawa vifaa vya uchaguzi ili viwe tayari kupelekwa kwenye vituo vya kupigia kura kesho Jumatatu. Bi Gloria Maina ndiye msimamizi mkuu wa uchaguzi katika eneo hilo na kituo cha kujumlisha kura ni shule ya upili ya wavulana ya Marigat.

  

Latest posts

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

NMS yakabidhi majukumu yake kwa kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi