Maafisa wa usalama wa Kenya wapokea mafunzo ya kukabiliana na Ugaidi kutoka kwa vikosi vya Marekani

Milio ya vilipuzi na ufyetuaji wa bunduki ilitawala siku ya Jumamosi wakati ubalozi wa Marekani ulipokuwa ukiendesha zoezi la kiusalama ambapo maafisa wa polisi wa humu nchini walipata mafunzo kabambe yaliyofadhiliwa na vikosi maalum vya marekani kuhusu kukabiliana na ugaidi.

Mafunzo hayo yaliyotekelezwa kwenye ubalozi wa marekani jijini Nairobi Jumamosi asubuhi, yalijumuisha mazoezi kuhusu hali za watu kuzuiliwa mateka na kushughulikia milipuko.

Also Read
Rais Kenyatta apokea stakabadhi za Mabalozi wapya katika ikulu ya Nairobi

Kwenye mazoezi hayo ya pamoja ya vikosi vya Kenya na marekani, maigizo ya milipuko, milio ya risasi na majeruhi yalikuwa sehemu ya mazoezi hayo yaliyowavutia wakenya.

Also Read
Asasi za usalama zasema hazitalegeza kamba kukabiliana na Ugaidi

Mazoezi hayo pia yalijumuisha kuwaondoa majeruhi na kuwapeleka kwenye hospitali zilizo karibu na vyumba vya dharura.

Mazoezi hayo yalipangwa kwa lengo la kuimarisha uwezo wa maafisa hao ambao huwa wa kwanza kufika kwenye matukio ya kigaidi ili kuwawezesha kushughulikia hali za dharura.

Also Read
Wizara ya Afya yatangaza visa vipya 573 vya maambukizi ya korona

Mazoezi hayo yalihudhuriwa na waakilishi wa serikali ya Kenya na shirika la usalama wa kidiplomasia la wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya marekani.

Haya yalikuwa makala ya sita ya mazoezi hayo yaliyotekelezwa na marekani na Kenya kuimarisha uwezo wa kukabiliana na ugaidi.

  

Latest posts

Ngirici aondoa kesi mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Waiguru

Tom Mathinji

Rais Museveni awaomba Wakenya msamaha

Tom Mathinji

Joyciline Jepkosgei apandishwa cheo hadi Sergeant baada ya ufanisi wa London Marathon

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi