Maafisa wa utawala kupiga jeki zoezi la usajili wa wapiga kura

Maafisa wa utawala wa serikali ya kitaifa watasaidia kikamilifu shughuli ijayo ya kitaifa ya usajili wa wapiga kura kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwezi Agosti mwaka 2022.

Waziri wa usalama wa kitaifa Dkt. Fred Matiang’i akihutubia wanahabari katika taasisi ya mafunzo ya kiufundi ya Borabu kaunti ya Nyamira, alisema wameshauriana kwa kina kuhusu jinsi watakavyosaidia shughuli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 17 mwezi huu.

Also Read
Aden Duale: Uchaguzi Mkuu sharti uandaliwe tarehe 9 mwezi Agosti mwaka 2022

Tumejadiliana kwa kina jinsi machifu na manaibu wao, watawajumuisha viongozi wote wakiwemo viongozi wa nyumba kumi na wazee wavijiji kuhakikisha watu wote waliohitimu katika sehemu wanazowakilisha, wanasajiliwa kuwa wapiga kura,” alisema Matiang’i.

Dkt. Matiang’i alisema maafisa hao pia watasaidia katika kuwatafuta raia wapatao 54,000 katika eneo la Nyanza pekee ambao hawajachukua kadi zao za vitambulisho vya kitaifa.

Also Read
Watafiti wa humu nchini wajizatiti kutafuta tiba ya kuumwa na nyoka

Alisema serikali imebadili mtindo wa kuhamasisha wakazi kujisajili kuwa wapiga kura ambapo sasa wanahusisha vitengo vyote vya viongozi kuanzia mashinani kwa ushirikiano na maafisa wa utawala wa serikali ya kitaifa NGAO ili kuhakikisha watu wengi iwezekanavyo wanajisajili kuwa wapiga.

Kulingana na waziri huyo maafisa wa utawala wako tayari kuhakikisha usalama wa wale wote wanawania nyadhifa za kisiasa popote ambapo watakuwa wakifanyia kampeni zao, iwapo hawatatumia lugha za matusi au kuzua ghasia.

Also Read
Ni rasmi Raila Odinga atawania Urais Katika uchaguzi mkuu ujao

“Tunapigia kurunzi maeneo matatu yanayikisiwa kuwa hatari, ambayo yanajumuisha Pwani, Kaskazini mashariki na Kaskazini mwa Rift Valley, ambayo yangali yanaripoti visa vya ukosefu wa usalama. Serikali imetoa rasilimali zaidi kwa maafisa wa usalama katika maeneo hayo kuhakikisha hali ya utulivu inadumishwa,” aliongeza Matiang’i

  

Latest posts

Riadha Kenya kuandaa seminaa kwa wanariadha Januari 21 kutangulia mashindano ya kitaifa

Dismas Otuke

Serikali yahakikisha usalama katika shule za Elgeiyo Marakwet

Tom Mathinji

Polisi wachunguza mauaji ya mwanamke aliyepatikana ndani ya sanduku

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi