Maambukizi ya COVID-19 yaongezeka hadi 39,427 baada ya visa vipya 243 kuthibitishwa

Wizara ya Afya imeripoti visa vipya 243 vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 na kufikisha 39,427, jumla ya idadi ya visa hivyo humu nchini.

Hii imetokana na upimaji wa sampuli 4,385 uliofanywa katika muda wa masaa 24 yaliyopita.

Kati ya visa hivyo vipya, 63 ni wanawake nao 179 ni wanaume, umri kutoka miezi mine hadi miaka 80.

Also Read
Mkutano kuhusu Ugatuzi Kung'oa nanga Jumanne Kaunti ya Makueni

Katika muda uo huo, wagonjwa 233 wamepona kutokana na COVID-19 na kuongeza idadi ya waliopona hadi 26,659.

Kati ya hao waliopona leo, 219 walikuwa katika mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani, nao 14 wakiruhusiwa kuondoka kutoka vituo mbali mbali vya afya humu nchini.

Also Read
Kijiji kizima chaendesha baada ya kula mzoga wa ngamia

Hata hivyo, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameripoti kuwa wagonjwa wengine watatu Wameaga dunia.

Kufikia sasa jumla ya wagonjwa 731 wameaga dunia tangu kuwasili kwa virusi hivyo humu nchini mnamo mwezi Machi mwaka huu.

Visa vipya 70 vya maambukizi hayo vimeripotiwa katika Kaunti ya Nairobi, ikifuatwa na Nakuru kwa visa 44, Trans Nzoia 30, Mombasa 15, Kisumu 15, Narok 13, Kiambu 11, Kericho 10, Kakamega 7, Machakos 6, Isiolo 4, Kajiado, Meru, Bungoma na Nandi visa vitatu kila moja, Uasin Gishu 2 nazo Kaunti za Bomet, Kirinyaga, Laikipia na Kilifi kisa kimoja kila moja.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi