Mabingwa wa NSL FC Tatanta waduwaza mabingwa watetezi wa ligi kuu Tusker FC 2-1

Mabingwa wa ligi kuu ya daraja ya kwanza NSL   msimu jana , Fc Talanta  wamezidisha masaibu ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tusker Fc baada ya kuwaadhibu mabao  2-1, katika uwanja wa Ruaraka Jumatano alasiri.

Wageni Talanta wamesali kutopoteza mechi wakipachika baoa la kwanza dakika ya 10 kupita kwa Francis Kahiro na kudumisha uongozi  huo hadi mapumzikoni.

Also Read
Nick Mwendwa kurejeshwa katika makao makuu ya DCI kuhojiwa zaidi

Kipindi cha pili wagema mvinyo walifanya mabadiliko kadhaa ya kiufundi yaliyozaa matunda baada ya Jackson Macharia kuwazawazishia wana mvinyo dakika ya 56,uongozi uliodumu kwa dakika 6 pekee kabla ya  Kahiro kuwarejesha tena wana mawasiliano uongozini  kwa goli la pili lililodumu hadi kipenga cha mwisho.

Tusker wamepoteza mechi zote mbili za ufunguzi huku Talanta wakiwa hawajashindwa mechi kufuatia mechi nne za msimu huu.

Also Read
Viboko wa Uganda kukabiliana na Ngorongoro Heroes ya Tanzania fainali ya CECAFA

Katika pambano jingine lililosakatwa katika uga wa kimataifa wa Kasarani,mabingwa mara 19 Gor Mahia walidumisha rekodi ya asilimia 100 baada ya kuwanyofoa Kariobangi Sharks mabao 2-0.

Chipikizi Benson Omala aliendelea kutesa akipachika bao la kwanza kwa Sir Kal kunako dakika 12 ,walioongoza hadi  mwishoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya  Peter Lwasa kuwaadhibu waajiri wake wa zamani kwa bao la pili dakika ya  83.

Also Read
Faith Kipyegon na Eliud Kipchoge wanawania tuzo ya wanariadha bora wa mwaka

Gor waliosakata mechi 3 wanakalia nafasi ya pili kwa pointi 9  sawa na City Stars iliyocheza mechi moja zaidi.

Fc Talanta wamezoa pointi 8 kutokana na mechi 4 katika nafasi ya 5.

 

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi