Mabondia watano wa Kenya waepuka mchujo wa kwanza mashindano ya Dunia AIBA

Mabondia watano wa Kenya wameepuka mchujo wa kwanza na wataanzia mchujo wa pili kwenye mashindano ya dunia mjini Belgrade Serbia.

Mabondia wa humu nchini wataanza kushuka ulingoni Jumanne kulingana na droo iliyoandaliwa Jumapili usiku.

David Karanja atakuwa bondia wa kwanza wa humu nchini kushuka ulingoni OKtoba 26 dhidi ya Luis Delgado wa Colombia katika uzani wa Fly huku Victor Odhiambo akizichapa dhidi ya Thapa Shiva kutoka India uzani wa Light Welter pia Jumanne.

Katika uzani wa Heavy Joshua Wasike wa Kenya atapigana katika mchujo wa kwanza na Uladzislau SMIAHLIKAU wa Belarus Jumanne kabla ya George Cosby Ouma kupimana nguvu na Mbelgiji Ziad El Mohor uzani wa light heavy.

Also Read
Hit Squad yaanza mazoezi kwa mashindano ya dunia nchini Serbia mwezi Oktoba

Siku ya Jumatano Oktoba 27 itakuwa zamu ya kapteini wa timu hiyo ya Hit Squad Nick Okoth kumenyana na Alexy De La Cruz wa Jamhuri ya Dominican katika mchujo wa kwanza uzani wa Light naye Hezron Maganga apigane na Riya Adel kutoka Jordan katika uzani wa Cruiser.

Boniface Mogunde wa Kenya atapimana nguvu na Alban Beqiri wa Alabania Oktoba 27 mchujo wa kwanza uzani wa light middle huku Shaffi Bakari anayeshiriki mashindano hayo kwa mara ya pili akiingia ulingoni kuvaana na Muhammet Sacli wa Uturuki katika mchujo wa kwanza uzani Bantam Oktoba 29 .

Also Read
Hit Squad kupimwa uzani tayari kwa mashindano ya Zone 3 mjini Kinsasha
Hit Squad mjini Belgrade Serbia 

Wanandondi watano watakaonzia mchujo wa pili ni Martin Maina atakayepigana kwa mara ya kwanza tarehe 30 mwezi huu katika uzani wa kilo 48,Martin Oduor atakayekabana koo na Nathan Lunata wa DRC Oktoba 28 katika uzani wa feather,Joseph Shigali ataanza Oktoba 28 katika raundi ya pili .

Edwin Okong’o atafungua kazi katika mchujo wa pili Oktoba 30 katika uzani wa kadri dhidi ya Aslami Suliman kisha Elly Ajowi pia aanze Oktoba 28 katika mchujo wa pili uzani wa super heavy dhidi ya Jakhon Qurbonov kutoka Tajistan.

Also Read
Hit Squad yaelekea Urusi kushiriki mashindano ya mwaliko ya EUBC

Kenya inawakilishwa na mabondia 13 wanaoshiriki katika vitengo vyote 13 vya mashindano hayo huku kwa mara ya kwanza kukiwa na  donge nono ya pesa ambapo mshindi wa dhahabu atatuzwa shilingi milioni 10,milioni  5  kwa washindi wa fedha na milioni 2 nukta 5 kwa washindi wa nishani za shaba.

Mashindano hayo yanayoandaliwa na shirikisho la ngumi ulimwenguni AIBA yataaanza Jumanne Oktoba 26 na kukamilika Novemba 4 .

  

Latest posts

Dismas Otuke

Omanyala ajiunga na National Police Service

Dismas Otuke

Rais wa zamani wa shirikisho la riadha ulimwenguni IAAF Lamine Diack afariki akiwa na umri wa miaka 88

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi