Shirika la maendeleo ya wanawake(MYWO) limepanga kuadhimisha miaka 70 tangu kubuniwa ,huku sherehe hizo zikipangwa kuandaliwa katika maeneo manane ya humu nchini yaliyokuwa mikoa ya zamani.
Kulingana na mwenyekiti wa shirika hilo Rahab Muiu, sherehe hizo zitaandaliwa katika maeneo ya Rift Valley,North Eastern,Eastern,Nyanza,Nairobi,Coast,Central na Western wakilenga kutumia fursa hiyo kutoa hamasisho kwa umma kuhusu majukumu na umuhimu wa kuwa mwanachama wa shirika hilo.
“MYWO tunasherehekea miaka 70 mwaka huu,na tunapanga kuwa na sherehe katika maeneo yote manane ambayo ni mikoa ya zamani ili kuelezea watu yale tunayofanya,historia yetu na ufanisi wetu ,kando na kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa kuwa mwanachama”akasema Rahab.

MYWO ilibuniwa mwaka 1952,na wake wa magavana wa wakoloni ,kama chombo cha kuunganisha kukuza na kuwawezesha wanawake kiuchumi na pia kisiasa.
Shirika hili lilisajiliwa rasmi mwaka 1955 na limekuwa katika mstari wa mbele kupigania haki za kina mama na kupigana dhidi ya dhuluma dhidi ya wanawake na wasichana.
Kwa sasa Mywo kama nji moja ya kusherehekea miaka 70 tangu kubuniwa itafungua jumba lake la pili jijini Mombasa, kando na ile ya Nairobi -Maendeleo Hoiuse na kupanua mradi wa wanawake kupata matanki ya maji kote nchini kupitia kwa mradi wa Water harvesting.
MYWO inawashirikisha wanachama 11 wa baraza kuu na waakilishi 47 waliochaguliwa kutoka kaunti zote,na viongozi 17,870 wa wadi na linajivunia wanachama milioni 4 .