Shirika la maendeleo ya wanawake limeshutumu matamshi ya kuwadhalilisha wanawake yanayotumiwa na baadhi ya wanasiasa kwenye mikutano yao ya kisiasa husasan katika siku za hivi punde.
Akiwahutubia wanahabari mapema Alhamisi katika afisi za shirika hilo ,mwenyekiti wa kitaifa Rahab Muiu amewataka wanasiasa kujitenga na matamshi ya udhalilishaji wanawake na lugha chafu,akirejea baadhi ya matamshi ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya wanasiasa wanaogemea mrengo wa Naibu Rais William Ruto.
“Hatutavumulia zaidi matusi na dhulma dhidi ya wanawake,matamshi yaliyotolewa kwenye video na Mkenya anayeishi Marekani na baadhi ya wanasiasa walio katika mrengo wa naibu Rais William Ruto ni ya kusikitisha na tunataka waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiangi’ na taasisi husika kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaoeneza siasa za chuki na matusi dhidi ya wanawake”akasema Bi Mwikali
Muiu pia ameshutumu vikali wale wanaomshambulia mama Ngina Kenyatta,mamake Rais Uhuru Kenyatta akisisitiza kuwa tofauti za kisiasa zapaswa kuwa kwa maswala wala sio matusi.
Muiu amemtaka naibu Rais kuomba msamaha kutokana na matamshi hayo yaliyotolewa na baadhi ya wafuasi wake na kupendekeza waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaoeneza cheche za matusi na kuwakosea heshima akina wanawake kwa jumla.
“Tunasema akina mama na wanawake waheshimiwe ,kila wakati na kila mahali wakati huu wa kampeini ,tunafunza nini watato wetu wakiskia matusi kama haya,wanasiasa hawa wakome matusi dhidi ya wanawake,na tunamtaka naibu Rais aombe msamaha kwa akina kote nchini”akasema Muiu
Kundi hilo la wanawake likiongozwa na mwakilishi wa akina mama kaunti ya Nairobi ,Esther Pasaris limeandamana hadi katika afisi za naibu Rais William Ruto kumtaka awachukulie sheria wanasiasa husika walio kwenye mrengo wake.