Magari ya uchukuzi wa umma kaunti ya Kilifi kupata vyeti vipya vya uzingativu wa Covid-19

Magari yote ya uchukuzi wa umma katika kaunti ya Kilifi kuanzia wiki ijayo yatahitajika kupata vyeti vipya vya uzingatiaji kanuni za ugonjwa wa Covid-19 ili kuruhusiwa kuhudumu.

Kamishna wa kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka aliagiza manaibu wa kamishna wote 9 katika eneo hilo kuyapa vyeti hivyo magari ya uchukuzi wa umma ambayo wenyewe na wahudumu wametimiza masharti hayo pekee.

Also Read
Kampeni Zakamilika Rasmi

Olaka alisema kamati ya kaunti ya kushughulikia ugonjwa wa Covid-19 imekubaliana na halmashauri ya kitaifa ya uchukuzi na usalama barabarani-NTSA kuondoa leseni za wahudumu wa magari ya utumishi wa umma ambao hawazingatii kanuni za wizara ya afya na maongozi yanayonuiwa kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo hatari.

Also Read
Kenya yanakili asilimia 6 ya kiwango cha maambukizi ya Covid-19

Kamishna huyo wa kaunti alikuwa akizungumza katika gereza kuu la Malindi wakati wa warsha kuhusu haki za wafungwa kupitia kanuni za kimsingi almaarufu sheria za Mandela.

Also Read
Viongozi wa Mlima Kenya waombwa kuwa makini katika siasa za urithi

Olaka alisema kamati hiyo pia imechukua hatua kukomesha mikusanyiko mikubwa ya watu kwenye mazishi na maeneo ya ibada.

“Tulikutana na kamati ya dini mbalimbali inayosimamia kaunti hii na kukubaliana swala la idadi ya watu kupita kiasi katika sehemu za kuabudu linasitishwa,” alisema Olaka.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi