Magari yenye nambari za usajili wa kigeni zanaswa kaunti ya Busia

Maafisa wa polisi katika kaunti ya  Busia wakishirikiana na vitengo vingine vya usalama, wamenasa magari 13 yenye nambari za usajili za nchi za kigeni yakihudumu katika mji wa Busia.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Busia Stephen Kimunya, amesema wakati wa oparesheni hiyo, magari yenye nambari za usajili za ubalozi pia yalinaswa.

Also Read
Kenya yaondoa marufuku ya Safari za ndege kuelekea Dubai

Kimunya amesema ni hatia kutumia magari yaliyosajiliwa na nambari za usajili za nchi za kigeni akisema inafanya taifa hili kupoteza ushuru, mbali na magari hayo kutumiwa kutekeleza uhalifu pamoja na shughuli za kigaidi.

Also Read
LSK: mahakama ndiyo mwamuzi wa mwisho kuhusu masuala ya kikatiba

Afisa huyo amesema oparesheni hiyo inayotekelezwa kote nchini itaendelea hadi magari hayo yote yatwaliwe.

Also Read
Nubian Li Ahalalisha Ndoa Yake

Christine Maliti, ambaye ni afisa wa forodha, amesema magari hayo ni tishio kwa usalama wa taifa hili, kwani habari zote kuhusu magari hayo zinapatikana katika nchi za kigeni.

  

Latest posts

Idadi ya wanawake wanaojifungua hospitalini kaunti ya Kilifi yaongezeka

Tom Mathinji

Waagizaji magari na pikipiki kutoka nje ya nchi kusajiliwa upya

Tom Mathinji

Serikali yapunguza bei ya pembejeo za Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi