Magawa Atungiwa Wimbo

Panya kutoka Tanzania kwa jina Magawa ambaye alipata umaarufu mwaka 2020 baada ya kutunukiwa medali kwa uwezo wake wa kutambua na kutegua mabomu ya ardhini na ambaye aliaga dunia juzi akiwa na umri wa miaka minane ametungiwa wimbo.

Mwanadada kwa jina Pendo Msegu ambaye alikuwa mwalimu wa panya Magawa ametunga wimbo wa kuenzi mnyama huyo. Kwenye wimbo huo, Pendo anamrejelea Magawa kama shujaa wa Tanzania ambaye aliweka alama Tanzania na duniani.

Also Read
Anderson .Paak atoa onyo

Video ya wimbo huo inamwonyesha Pendo akicheza na panya wengine na akipeperusha bendera ya Tanzania. Pendo anafanya kazi na shirika kwa jina “Apopo” ambalo linajihusisha na kutoa mafunzo kwa wanyama kama vile panya kutambua na kuharibu mabomu.

Also Read
"Nitamheshimu milele", Sarah kuhusu Harmonize

Anasema kwenye wimbo wake kwamba panya Magawa alikuwa mmoja wa panya ambao walikuwa wameafikia makubwa kwani alisaidia katika kutambua na kuharibu mabomu ya kutegwa ardhini zaidi ya 100.

Taarifa za kifo cha panya huyo zilitolewa tarehe 11 mwezi Januari mwaka huu wa 2022 na shirika la Apopo kupitia akaunti za shirika hilo za mitandao ya kijamii. Kulingana na shirika la Apopo afya ya Magawa ilidhoofika kwa siku chache na akafa akiwa nchini Cambodia.

Also Read
Filamu za Kenya katika jukwaa la kimataifa

Magawa alitimiza umri wa miaka minane mwezi Novemmba mwaka 2021 na aliandaliwa sherehe ya siku ya kuzaliwa. Miaka minane ndio umri mkubwa zaidi ambao panya anaweza kuishi.

  

Latest posts

Rais Samia Alivyosherehekewa Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

Marion Bosire

Azimio la Bien Barasa Mwaka Huu

Marion Bosire

Anne Kansiime Afiwa na Baba Mzazi

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi