Magoha: Asilimia 100 ya wanafunzi wamejiunga na kidato cha kwanza

Waziri wa elimu Gerorge Magoha anasema wizara hiyo sasa inaweza kubaini kuwa asili-mia 100 ya wanafunzi 1,171,265 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza baada ya kufanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane wa 2020 wamejiunga na shule za upili.

Also Read
Rais Kenyatta azindua idara mpya ya serikali itakayosimamia utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu

Alisema hayo wakati wa kukamilisha kwa shughuli za rasmi za wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule zote za umma.

Kufikias sasa jumla ya wanafunzi 1,129,637 ambao wanaashiria (asilimia 98) wamejiunga na kidato cha kwanza katika shule zote za umma na za kibinafsi.

Also Read
Simiyu Robinson Wanjala ndiye mwanafunzi bora wa mtihani wa KCSE 2020

Wanafunzi 2,658 wamejisajili kufanya tena mtihani wa kitaifa wa darasa la nane. Kadhalika, wanafunzi 11,213 wamejiunga na vyuo vya mafunzo ya kiUfundi huku wanafunzi 1,193 wakiwa wamehama makwao au kufariki.

Also Read
Magoha: Wakati umewadia wa kufungua tena Taasisi za Elimu

Magoha alisema kaunti 17 zilifanikiwa kuandikisha kiwango cha asili-mia 100, cha wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza huku kaunti 11 kati yao zikirekodi zaidi ya asili-mia 100 ya kiwango hicho.

  

Latest posts

Wakazi wa Nandi ya kati wahimizwa kushirikiana na polisi kukabiliana na uhalifu

Tom Mathinji

Serikali yahimizwa kutoa mikopo ya HELB kwa wanafunzi wa vyuo vya kibinafsi

Tom Mathinji

Mahakama iko tayari kwa kesi za uchaguzi mkuu ujao asema Jaji mkuu Martha Koome

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi