Magoha: Serikali haitabatilisha agizo lake kuhusu utumiaji wa mabasi ya shule.

Kwenye taarifa kwa vituo vya habari, Prof. Magoha alisema wizara hiyo imegundua kuwa baadhi ya wasimamizi wa shule wangali wakiruhusu utumiaji wa mabasi ya shule kwa shughuli zisizohusiana na masomo.

“Wizara ya elimu imepata habari kwamba baadhi ya wasimamizi wa shule wanaruhusu mabasi ya shule yatumie kwa shughuli ambazo si za masomo,” alifoka Magoha.

Also Read
Wahudumu wa boda boda watajwa kuwa washiriki wakuu wa unyanyasaji wa kijinsia

Waziri amewatahadharisha wasimamizi hao wa shule kukoma kukodisha mabasi hayo kwa shughuli zisizostahili.

Aidha  Magoha amesema baadhi ya shule zinakosa kuzingatia kanuni za wizara ya afya kuhusu udumishaji wa umbali baina ya watu kwenye magari hali inayowaweka wanafunzi katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19.

Also Read
COVID-19: Watu 427 zaidi waambukizwa huku mgonjwa mmoja akiaga dunia

Kwa mujibu wa waziri huyo, wasimamizi hao wa shule ni sharti wahakikishe mikakati ya wizara ya afya ya kuzuia msambao wa ugonjwa wa COVID-19 inazingatiwa kikamilifu.

“Wakati wa kuwasafirisha wanafunzi, wasimamizi wa shule wanapaswa kuhakikisha masharti ya wizara ya afya ya kuzuia kusambaa kwa Covid-19 yanazingatiwa kikamilifu,” aliagiza Magoha.

Also Read
Afisa wa zamani wa KDF afungwa jela kwa kosa la ulaghai

Waziri amesema hatua kali itachukuliwa dhidi ya watu au makundi ya watu watakaopatikana wakikiuka maagizo kuhusu utumiaji wa mabasi ya shule

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi