Magoha: Serikali iko tayari kutekeleza mtaala wa CBC

Waziri wa elimu amekanusha madai kuwa walimu nchini hawako tayari kutekeleza mtaala mpya wa elimu wa CBC,akiongeza kuwa walimu wamepata mafunzi na wako tayari kwa utekelezaji wa mtaala huo mpya.

Magoha aliwakosoa wale wanaopania kuwasilisha kesi mahakamani kusitisha utejkelezaji wa mtaala huo mpya wa CBC.

Alisema mtaala huo utanufaisha pakubwa sekta ya elimu nchini.Matamshi yao yanajiri kufuatia shtuma za baadhi ya wazazi kuwa gharama ya utekelezaji wa mtaala huo ni ghali.

Also Read
Kang'ata atishia kuishtaki serikali ya kaunti ya Murang'a kwa kusitisha kambi za matibabu

Akikubaliana na hisia zilizowasilishwa,waziri alikaribisha maoni na mapendekezo ambayo yanaweza kuboresha zaidi mtaala huo.

Alisema mtaala huo mpya utaboresha pakubwa sekta ya elimu nchini. Kuhusu gharama ya mtaala huo ,waziri alisema kuwa kulingana na takwimu za kimataifa,gharama ya utekelezaji huo ni ya kadri.

Alisema hayo leo alipokutana na chama cha wahariri nchini.

Also Read
Uchaguzi mdogo wa Seneta wa Machakos wang’oa nanga kwa utaratibu

Wakati huo huo Serikali imetoa wito kwa wazazi kutekeleza majukumu yao katika elimu ya watoto wao.

Akiongea Jumanne  asubuhi Jijini Nairobi wakati wa hafla ya kuelezea mafanikio katika utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu wa CBC,katibu mwandamizi katika wizara ya elimu Sarah Rutto alisema wazazi wanawajibu muhimu katika masomo ya watoto wao.

Dkt. Rutto hatahivyo alitoa wito wa majadiliano baina ya shule na wazazi kuhusiana na masomo ya watoto wao.

Also Read
Mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE kufanywa mwaka ujao jinsi ilivyopangwa

Kuhusu swala la mafunzo kwa walimu, Dkt. Rutto alisema tayari walimu 228,000 wa shule za msingi wamepokea mafunzo kuhusiana na mtaala hup mpya .

Mwakilishi wa tume ya kuwaajiri walimu nchini Rueben Ndamburi alisema tume hiyo inapanga kutoa mafunzo kwa walimu wengine 106,000 wa shule za msingi.

  

Latest posts

Aliyekuwa mtangazaji Mwanaisha Chidzuga ajitosa katika ulingo wa siasa

Tom Mathinji

#KisaChangu: Dr Mukhisa Kituyi kuwania urais ili kukamilisha safari ya ukombozi

John Madanji

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi