Mahakama kutoa uamuzi leo kuhusu rufaa saba za kupinga BBI

Jopo la majaji watano leo linatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu rufaa saba za kupinga mpango wa marekebisho ya katiba wa BBI.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Naibu msajili wa kitengo cha kesi za kikatiba na haki za binadamu Njeri Thuku alisema uamuzi huo utatolewa kwa njia ya video.

Also Read
Mudavadi atoa wito wa mdahalo wa kitaifa kuhusu mswada wa BBI

Majaji Joel Ngugi, George Odunga, Jarius Ngaah, Janet Mulwa, na Chacha Mwita wamepangiwa kuamua iwapo kura ya maamuzi itaandaliwa kuhusu marekebisho yanayopendekezwa ya kikatiba.

Mahakama Kuu mwezi Februari mwaka huu, ilisimamisha Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) kuandaa kura ya maamuzi hadi kesi zote za kupinga mchakato huo zitakaposikizwa na kuamuliwa.

Also Read
Raila, Gavana Kingi wafokeana hadharani kuhusu chama cha Pwani

Walalamishi ni pamoja na mtaalum wa maswala ya kiuchumi David Ndii, Chama cha kitaifa cha Wauguzi, Chama cha Thirdway Alliance na shirika la kiislamu la Muhuri.

Also Read
Jopo la kusaili makamishna watakaojiunga na IEBC lazinduliwa

Mswada wa marekebisho ya katiba tayari imepitishwa na mengi kati ya mabunge ya kaunti, Bunge la Kitaifa na lile la Seneti na sasa uamuzi unaosubiriwa utatoa mwelekeo iwapo mswada huo uko huru kuelekezwa debeni kwa kura ya maamuzi.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi