Mahakama kuu yabatilisha sheria 24 zilizopitishwa na bunge la taifa bila kuhusisha lile la Senate

Mahakama kuu jiji Nairobi Alhamisi ilibatilisha sheria 24 zilizopitishwa na bunge la taifa bila ushiriki wa bunge la Senate.

Uamuzi huo wa jopo la majaji watatu waliojumuisha Jairus Ngaah, Anthony Ndung’u na Teresiah Matheka  ulisema bunge la Senate haliwezi kupuuzwa kutokana na jukumu lake la kikatiba katika utungaji sheria.

Hata hivyo mahakama hiyo ililipa afueni bunge la taifa kwa kuahirisha tangazo la kubatilisha sheria hizo kwa miezi tisa ili lirekebishe hali hiyo.

Also Read
Wanafunzi warejea shuleni baada ya miezi sita ya kukaa nyumbani

Bunge la Senate liliwasilisha rufaa katika mahakama kuu mwaka jana kupinga uhalali wa sheria zilizopitishwa na bunge la taifa bila kuhusisha bunge la Senate zinahusu kaunti moja kwa moja na hivyo basi mchango wao ulihitajika kama ilivyoratibishwa kisheria.

Miongoni mwa sheria zilizobatilishwa na sheria kuhusu halmashauri ya usambazaji dawa nchini-KEMSA ambayo ilizizuia serikali za kaunti kununua dawa kutoka taasisi nyingine yoyote isipokuwa KEMSA.

Also Read
Haji akariri kwamba wahusika wa kashfa ya KEMSA watachukuliwa hatua

Sheria nyingine zilizobatilishwa ni pamoja na  mswada wa marekebisho ya sheria kuhusu halmashauri ya usambazaji dawa, ile ya marekebisho ya sheria kuhusu wadhamini wa mali, sheria ya marekebisho kuhusu masoroveya wa ujenzi, sheria ya kuhusu utumiaji usiofaa wa tarakilishi na  uhalifu wa kimtandao na sheria kuhusu ugavi wa pesa za hazina ya usawazishaji.

Also Read
Maafisa wawili wa polisi wafyatuliana risasi wakizozania mwanamke

Zingine ni sheria kuhusu vyama vya akiba na mikopo,sheria kuhusu huduma ya taifa kwa vijana ,sheria kuhusu sekta ya michezo na sheria ya kuhusu tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa.

Majaji hao waliagiza kwamba mabunge yote mawili yapasa kujihusisha katika kuidhinisha miswada inayohusu mfumo wa ugatuzi na kaunti.

  

Latest posts

Mauaji ya mwanaume mmoja yazidisha taharuki Ol Moran

Tom Mathinji

IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

Tom Mathinji

COVID-19 yavuruga mbinu za upangaji uzazi hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi