Mahakama ya ICC yamfunga miaka 25 gerezani, aliyekuwa kiongozi wa waasi wa Uganda Dominic Ongwen

Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Uganda Dominic Ongwen amehukumiwa miaka 25 gerezani na Mahakama ya Kimataifa ya jinai (ICC).

Ongwen alikuwa anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo ubakaji, kutumisha watu kimapenzi, utekaji nyara wa watoto, kutesa watu na mauaji.

Mahakama hiyo ya Kimataifa iliyoko Mjini Hague, nchini Uholanzi imetangaza Alhamisi kwamba Ongwen amepatikana na jumla ya makosa 61 aliyotekeleza Kaskazini mwa Uganda kati ya tarehe moja Julai mwaka wa 2002 na tarehe 31 mwezi Disemba mwaka wa 2005.

Also Read
Suluhu azuru Uganda kwa mwaliko wa Museveni

“Muda aliokuwa amezuiliwa kati ya tarehe nne Januari mwaka wa 2015 na tarehe sita Mei mwaka wa 2021 utapunguzwa kutoka kwa muda wa kifungo alichopewa,” ikasema mahakama ya ICC baada ya kutoa uamuzi huo.

Also Read
Marekani yataka kuchunguzwa kwa ghasia za uchaguzi nchini Uganda

Mahakama hiyo imesema kwamba ilichunguza kisa kimoja baada ya chengine kati ya vyote 61 ambavyo Dominic Ongwen alishtakiwa kwavyo na ikatosheka na ushahidi uliopo kwamba alitekeleza uhalifu huo.

Also Read
Liberia yaitisha usaidizi wa Marekani kutegua mauaji tatanishi ya maafisa watatu

Hata hivyo mahakama hiyo imetoa ruhusa kwa pande zote mbili kukata rufaa kuhusu uamuzi huo iwapo hawajatosheka.

  

Latest posts

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Ethiopia yakaribisha wito wa kurejelewa mazungumzo na majirani wake kuhusu bwawa katika mto Nile

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi