Mahakama ya Meru yasitisha huduma kutokana na maambukizi ya COVID-19

Huduma katika mahakama za Meru zimesitishwa kwa sababu ya msambao wa virusi vya Korona.

Kulingana na arifa iliyotolewa na Jaji Mkuu David Maraga, baadhi ya wafanyakazi katika mahakama hiyo, mawakili na wafanyakazi wao walithibitishwa kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo na kusababisha kufungwa kwa mahakama hiyo.

Also Read
Maraga asifu mfumo wa dijitali wa shughuli za mahakama

Agizo hilo litakaloanza kutekelezwa kesho litadumu kwa muda wa wiki mbili ili kutoa nafasi kuwekwa kwa mikakati ifaayo kuzuia msambao zaidi.

Also Read
Kenya yaripoti visa vipya 486 vya maambukizi ya COVID-19

“Tumeamua kwamba shughuli na huduma zote za mahakama zinazohusu watu kutangamana katika Mahakama ya Meru zisimamishwe kwa siku 14 kuanzia Jumatatu tarehe 23 Novemba, 2020,” amesema Jaji Mkuu.

Hata hivyo, Maraga amekubali kesi za dharura kusikilizwa kupitia video.

Also Read
Wizara ya Afya yanakili visa 394 vya COVID-19 na vifo 14

Ameongeza kuwa shughuli zitarejelewa katika mahakama hiyo baada ya maafisa kupimwa na kuthibitishwa kwamba hawana virusi vya Korona na maafisa wa wizara ya afya.

  

Latest posts

Uhaba wa maji wakumba kaunti ndogo ya Lagdera baada ya kukauka kwa vidimbwi

Tom Mathinji

Magoha: Serikali haitabatilisha agizo lake kuhusu utumiaji wa mabasi ya shule.

Tom Mathinji

Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi