Mahakama ‘yaidhinisha’ mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Matungu Justus Murunga

Familia ya aliyekuwa Mbunge wa Matungu Justus Murunga sasa inaweza kuanza utaratibu wa mazishi baada ya Mahakama kuondoa agizo la kusimamisha mazishi hayo.

mwili wa Murunga sasa utafanyiwa maziko tarehe 5 mwezi ujao. Awali, Mahakama ilitoa agizo la kusimamisha maandalizi ya mazishi ya Murunga hadi kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi iliyowasilishwa na mwanamke anayedai kuwa mpenzi wa mwendazake.

Also Read
Migogoro kati ya binadamu na wanyamapori yaongezeka kaunti ya Homa Bay

Wajane wawili wa Murunga, kupitia kwa wakili wao Patrick Lutta, pia walielekea Mahakamani kutaka agizo hilo liondolewe.

Christabel Murunga na Grace Murunga walihoji kuwa kusimamishwa kwa mazishi ya mume wao kunaendelea kuisababishia familia hiyo masaibu zaidi.

Agnes Wangui aliwasilisha kesi Mahakamani akidai kuwa Murunga ndiye baba wa watoto wake wawili na kuomba uchunguzi wa DNA ili kuhakikisha madai yake, ombi ambalo lilikubaliwa.

Also Read
Mkataba kati ya benki ya Stanbic na Serikali ya kaunti ya Meru kuwanufaisha wanabiashara

Hatua hiyo ilisababisha kuahirishwa kwa hafla ya mazishi ya mbunge huyo yaliyokuwa yafanyike tarehe 28 mwezi huu, huku Wangui akihoji kuwa amekuwa kwenye mahusiano na Murunga kwa miezi saba hadi kupata watoto wawili pamoja naye; mvulana na msichana.

Also Read
Maafisa wa IEBC kufika bungeni kueleza kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu

Mwanamke huyo pia alifichua madai kwamba wawili hao walikuwa na mipango ya kuoana kulingana na tamaduni za Agikuyu kabla mbunge huyo kufariki ghafla.

Wangui anadai kwamba alikuwa amenunuliwa shamba katika eneo la Karen na mbunge huyo ambaye pia alikuwa anapanga kumjengea nyumba.

  

Latest posts

Rais Kenyatta amwomboleza Nancy Karoney, dadake waziri wa ardhi Farida Karoney

Tom Mathinji

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi