Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Mahakama kuu imetoa agizo la kumzuia mkurugenzi wa huduma za jiji la Nairobi NMS, luteini  Jenerali Mohamed Badi kuhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri. Vile vile Mahakama hiyo imemzuia Badi kutekeleza majukumu ya baraza la mawaziri.

Also Read
Wizara ya Afya yatangaza visa vipya 984 vya maambukizi ya korona

Akitoa uamuzi huo katika mahakama ya Milimani, Jaji wa mahakama kuu Anthony Mrima alitupilia mbali uamuzi wa rais  Uhuru Kenyatta ambao ulimteua na kumjumuisha  Badi katika mikutano ya baraza la mawaziri.

Also Read
Jamii zisizojiweza kunufaika na msaada wa bima ya afya kaunti ya Migori

Katika kesi hiyo, mbunge wa  Kandara Alice Wahome alifika mahakamani kupinga uhalali wa kikatiba wa kumteua na kumjumuisha Badi katika mikutano na kamati za baraza la mawaziri.

Also Read
Mfanyibiashara wa Nyeri aliyetuhumiwa kwa mauaji ya mwanawe ameaga dunia

Kabla ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya NMS, Badi alikuwa mkuu wa mafunzo kwa kikosi cha jeshi la wanahewa katika chuo cha ulinzi Jijini Nairobi.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi