Mahakama imesimamisha kwa muda wa siku kumi kampuni moja ya Uganda Sarrai Group, kuendelea na shughuli katika kiwanda cha sukari cha Mumias kusubiri kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi iliyowasilishwa mahakamni.
Hayo yamejiri huku wakulima wa Gakwamba wakifika mbele ya jaji Wilfrida Okwani wakitaka kujumuishwa kwenye kesi hiyo.
Kampuni hiyo kutoka uganda ilishinda zabuni ya kukondisha kiwanda hicho licha ya kuwa kampuni hiyo ilikuwa ya tatu kwa kiwango cha shilingi bilioni 11.5 cha pesa ilichotangaza nia ya kulipa kuendesha kiwanda hicho.
Alhamisi mahakama ya kakamega iliweka kando maagizo ya mahakama ya hapo awali yaliyoipa kampuni hiyo idhini ya kuendelea na shughuuli za kiwanda hicho ilipobainika kwamba agizo hilo la mahakama lilihitilafiana na agizo lingine lililokuwa limetolewa mwezi Desemba.
Wakati huohuo mhasibu wa shirika la reli nchini Patrick Kareithi Ndegwa ameshtakiwa kwa kuhitilafiana na mfumo wa ulipaji mishahara wa shirka la reli nchini kwa kuondoa kwenye mshahara wake pesa zote alizopaswa kukatwa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Ni tukio lililosababishia shirika hilo hasara ya shingi 317,500.
Alipofika mbele ya hakimu Bernard Ochoyi, Patrick alikanusha madai hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki 3 au pesa taslimu shilingi laki mbili.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 28 mwezi huu.