Mahakama yasitisha mgomo wa matabibu uliodumu siku 70

Matabibu humu nchini wamesitisha mgomo wao miezi mawili kufuatia agizo la mahakama. Mwenyekiti wa chama cha matabibu, Peter Wachira ameagiza maafisa hao kurudi kazini.

Matabibu waligomea kazi kwa siku-70 kushinikiza serikali ishughulikie matakwa yao. Wachira amesema matabibu walisusia kazi kutokana na mazingira duni ya kikazi.

Alilalamikia hatua ya kuwalazimisha kurejea kazini na ilhali malalamishi yao hayajashughulikiwa ipasavyo.

Mahakama ya kushughulikia maswala ya wafanyikazi na waajiri kupitia kwa jaji Maureen Onyango ilitoa agizo hilo siku ya Jumatatu huku ikiwataka kurejea kazini haraka iwezekanavyo

Wakati huo huo, wahudumu wa afya katika kaunti ya Busia wametamatisha mgomo wao baada ya zogo la karibu siku 72.

Hii inafuatia makubaliano kati ya serikali ya kaunti, chama cha matibabu nchini na chama cha taifa cha wauguzi.

Gavana wa Busia Sospeter Ojaamong alisema serikali yake haitawachukulia hatua za nidhamu wahudumu wa afya ambao watarejea kazini na akahakikishia kuwalipa mishahara yao yote.

Akiongea baada ya kufanya mashauri na vyama hivyo vya wahudumu wa afya, Ojaamong alipongeza hatua hiyo ya wahudumu hao wa afya, akisema hizo ni habari za kuridhisha kwa wakazi ambao hawajakuwa wakipokea huduma za afya.

Siku ya Jumatatu, wauguzi na wahudumu wengine wa afya katika kaunti ya Mombasa, walirejea kazini baada ya kushiriki mgomo kwa muda wa miezi mitatu.

Zaidi ya wananchama 1000 wa chama cha wauguzi nchini KNUN, kile cha matabibu nchini,KUCO na chama cha maafisa wa maabara, walianza mgomo tarehe 15 mwezi Novemba mwaka jana baada ya serikali ya kaunti ya Mombasa kudinda kushughulikia matakwa yao.

  

Latest posts

Magoha: Serikali haitabatilisha agizo lake kuhusu utumiaji wa mabasi ya shule.

Tom Mathinji

Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 1,259 vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi