Mahojiano ya kuwasaka makamishna wa IEBC kuendelea leo

Shughuli ya kuwasaili waliopeleka maombi ya kuteuliwa kuwa makamishna wa tume ya IEBC inatarajiwa kuendelea leo mbele ya Jopo la usaili la tume hiyo katika Jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta (KICC).

Also Read
Visa 1,263 vipya vya COVID-19 vyathibitishwa hapa nchini

Mwenyekiti wa Jopo hilo Dkt. Elizabeth Muli amesema shughuli hiyo itaendelea hadi tarehe 22 mwezi huu.

Alisema mahojiano hayo yamekuwa yakifanyika hadharani kuambatana na ibara ya tatu ya ratiba ya kwanza ya sheria ya mwaka 2011 kuhusu IEBCna pia kwa kuzingatia kanuni za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wCovid-19.

Jopo hilo linatarajiwa kuwahoji jumla ya watu 36 ambao wanawania nyadhifa nne za Makamishna wa IEBC.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi