Majambazi wawili wauawa na polisi mtaani Eastleigh

Majambazi wawili waliokuwa na silaha waliuawa kwa kupigwa risasi wakati wa jaribio lao la kuvunja duka moja la vyuma lililoko mtaa wa Eastleigh, jijini Nairobi.

Idara ya upelelezi wa Jinai inasema maafisa wa kituo cha polisi cha Pangani walizima jaribio hilo la wizi wa kimabavu baada ya kupashwa habari na raia wema.

Also Read
Raia watatu wa kigeni wanaswa na pesa bandia Ruiru

ā€¯Maafisa wa polisi walipashwa habari kuhusu wizi huo na kisha kufika mahali hapo na kuwapiga risasi majambazi wawili. Awali majambazi hao waliwasili katika duka na gari aina ya pickup kutekeleza wizi huo,” ilisema idara ya DCI.

Also Read
Kenya yatajwa kivutio bora zaidi cha watalii duniani mwaka 2020

Maafisa hao wanawaandama majambazi wengine wane ambao walitoroka na majeraha ya risasi kufuatia makabiliano makali na maafisa wa polisi.

Sita hao walikuwa wamewasili kwenye duka la vyuma la Jamarat lililoko kwenye barabara ya Nne mtaa wa Eastleigh.

Also Read
Naibu Rais Dkt. William Ruto atoa wito wa haki katika vita dhidi ya Ufisadi

Bastola moja iliyokuwa na risasi tatu, na pia silaha nyingine butu vilipatikana mahala pa tukio.

Aidha, matangi mawili ya maji pia yalipatikana mahala hapo.

  

Latest posts

Rachier airai wizara ya michezo kuinusuru Gor Mahia FC kupitia Sports Fund

Dismas Otuke

Aden Duale: Uchaguzi Mkuu sharti uandaliwe tarehe 9 mwezi Agosti mwaka 2022

Tom Mathinji

Mudavadi asema taifa hili halipaswi kushuhudia ghasia kama zile za mwaka 2007

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi