Majaribio ya kuteua kikosi kwa michezo ya Commonwealth yaahirishwa

Majaribio ya kitaifa kutea kikosi cha Kenya kwa michezo ya jumuiya ya madola yaliyokuwa yaandaliwe baina ya Mei 20 na 21 katika uwanja wa Kasarani yameahirishwa.

Also Read
Wakenya kuwinda nishani katika siku ya mwisho ya mashindano ya dunia nchini Poland Jumapili

Chama cha riadha Kenya kimeahirisha uteuzi huo na sasa utaandaliwa kwa pamoja na majaribio ya kutafuta timu itakyishiriki mashindano ya dunia.

Majaribio ya kitaifa kuchagua timu ya Kenya kwa mashindano ya dunia mjini Oregon Marekani yataandaliwa baina ya Juni 24 na 25 .

Also Read
Timu ya Kenya ya riadha kwa mashindano ya dunia yaondoka kwenda Belgrade

Kenya imepewa fursa ya kutuma kikosi cha wanariadha 50 kwa michezo ya jumuiya ya madola itakayoandaliwa mjini Birmingham Uingereza .

Also Read
Raila Odinga aondoka nchini kuelekea Uingereza

Mashindano ya riadha katika makala ya 22 ya michezo ya jumuiya ya madola yataandailiwa kati ya Agosti 2 na 7.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi