Majasusi wanamsaka afisa wa polisi mwanamke kwa kuwaua watu wawili

Majasusi wanamtafuta afisa mmoja wa polisi mwanamke aliyempiga risasi na kumuua mtu mmoja katika eneo la Juja siku moja tu baada ya kumuua afisa mwenzake wa polisi kaunti ya Nakuru. 

Kwa mujibu wa majasusi hao Caroline Kagongo aliye na cheo cha konstabo anayeshukiwa kumuua afisa wa polisi konstabo John Ogweno, alimuua kwa kumpiga risasi mtu mmoja Jumatatu jioni.

Also Read
Wizara ya elimu kutangaza kalenda ya masomo ya mwaka 2021 katika siku 14 zijazo

Mshukiwa huyo anayesemakana kuwa amejihami na hatari, yuko mafichoni baada ya kumuua konstabo Ogweno.

“Tunawatahadharisha umma hususan wanaume kuwa waangalifu dhidi ya afisa huyo,” walisema majasusi hao.

Kwa mujibu wa majasusi hao, afisa huyo aliyetoroka na bunduki ya Ogweno aina ya Ceska ikiwa na risasi, alimhadaa mwanaume mmoja kuingia katika hoteli ya Dedamax katika mtaa wa Juja siku ya Jumatatu saa kumi alasiri.

Also Read
Kundi la vijana Nakuru lazindua mpango wa kunyunyizia kemikali taasisi za umma

Baadaye aliondoka katika chumba cha hoteli hiyo mwendo wa saa sita usiku na akatorokea kusikojulikana na kumwacha marehemu kitandani.

Also Read
Baraza la vyombo vya habari kuchunguza upya mwongozo kuhusu uchaguzi

Mwanamke huyo alimhadaa mwanaume huyo kuingia katika chumba hicho cha hoteli kabla ya kumpiga risasi kichwani.

Aliwadanganya wahudumu wa hoteli hiyo kuwa alikuwa akienda dukani na kasha kutoroka.

Majasusi wamewahimiza wananchi kutomwamini mwanamke huyo na kupiga ripoti kwa polisi watakapomwona.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi