Majeshi ya Uingereza kuondoa vilipuzi vilivyosalia Laikipia na Samburu

Kitengo cha mafunzo kwa wanajeshi wa Uingereza humu nchini Kenya -(Batuk), kimeanzisha zoezi la kuokota vifaa vyote ambavyo havijalipuka kwenye kaunti za Laikipia na Samburu katika juhudi za kuhakikisha kwamba maeneo hayo ni salama.

Akiongea katika eneo la mafunzo huko Archers Post, kaunti ya Samburu, naibu kamanda wa kitengo cha (Batuk) nchini Kenya Luteni Kanali Finlay Bibby, alisema zoezi la kusafisha eneo hilo la mafunzo, linatekelezwa kwa pamoja na maafisa wa vikosi vya ulinzi wa Kenya -(KDF), kwa vile wanajeshi wa mataifa haya mawili hupewa mafunzo kwa pamoja.

Also Read
Serikali yatakiwa kuwakamata viongozi wanaofadhili ujangili Baringo

Alisema shughuli ya kusafisha eneo hilo la mafunzo ni zoezi la kila mwaka, na kwamba shughuli hiyo itaendelezwa kadri ambavyo maafisa wa kitengo cha (Batuk) wataendelea kuwa nchini Kenya, ili kuhakikisha mazingira salama kwenye kambi za mafunzo, hata nyakati ambapo maafisa wa kijeshi hawapo.

Also Read
Maafisa watano wa KDF washtakiwa kwa kupokea hongo kutoka kwa makurutu

Wakati wa zoezi hilo la mwishoni mwa juma, Luteni Bibby alidokeza kwamba maafisa wa kijeshi walipata zaidi ya vifaa 50 ambavyo havijalipuka na ambavyo vingesababisha maafa miongoni mwa wakaazi na hata wanyama pori.

Also Read
Afisa wa KDF ashtakiwa kwa kumnajisi msichana wa miaka 16 Nyeri

Aidha, kamanda huyo wa jeshi la Uingereza, alisema ni jukumu lao kuhakikisha kwamba maeneo ya mafunzo yanaachwa salama hata baada ya shughuli za mafunzo kukamilika.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi