Makala ya 32 ya Olimpiki yaanza rasmi jijini Tokyo huku zaidi ya wachezaji 11,000 wakishiriki

Makala ya 32 ya michezo ya Olimpiki yanaanza Ijumaa na kukamilika tarehe 8 mwezi ujao mjini Tokyo Japan baada ya kuahirishwa Kutoka mwaka jana kutokana na janga la covid 19.

Japan inaandaa Olimpiki kwa mara ya pili baada ya kuwa mweyeji wa michezo hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 1964.

Also Read
Malkia Strikers yaendeleza mazoezi Kasarani kujiandaa kwa Olimpiki
Uwanja wa Olympic mjini Tokyo 

Michezo hiyo itawashirikisha wanamichezo zaidi ya wanamichezo 11,238 kutoka nchini 204 wanachama wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC wakishindana katika michezo 339 ikiwa na katika fani 33 za spoti.

Kenya inawakilishwa na wanamichezo 85 watakaoshindana katika fani 6 za Voliboli,raga kwa wachezaji 7 upande,ndondi,riadha ,taekwondo na uogeleaji.

Also Read
Malkia Strikers waanza kambi ya siku nne Mombasa ya nyanda za chini
Mwonekano wa  ndani ya  Uwanja wa  Olimpic Tokyo 

Washiriki 40 wa Kenya ni wanariadha huku voliboli ikiwa na washiriki 14 wakati raga ya wanaume na wanawake ikiwa na washiriki 24 ,mchezaji taekwondo mmoja,waogeleaji wawili na mabondia wane.

Also Read
Chipukizi wa miaka 19 Athing Mu wa Marekani ndiye bingwa wa Olimpiki katika mita 800
Mji wa Tokyo

Timu ya voliboli kwa wanawake maarufu kama malkia strikers ndiyo itakuwa ya kwanza kuingia uwanjani Jumapili Julai 25 dhidi ya Dominican Republic ,ikifuatwa na timu raga ya wanaume shujaa itakayocheza mechi mbili za kundi A mapema Jumatatu dhidi ya USA na Afrika Kusini.

 

  

Latest posts

Wakazi wa Nandi ya kati wahimizwa kushirikiana na polisi kukabiliana na uhalifu

Tom Mathinji

Serikali yahimizwa kutoa mikopo ya HELB kwa wanafunzi wa vyuo vya kibinafsi

Tom Mathinji

Mahakama iko tayari kwa kesi za uchaguzi mkuu ujao asema Jaji mkuu Martha Koome

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi