Malala apokonywa uongozi wa wachache Seneti na kurithiwa na Madzayo

Seneta wa Kaunti ya Kakamega Cleaphas Malala amebanduliwa kutoka kwa wadhifa wa Naibu Kiongozi wa wachache katika Bunge la Seneti.

Kwenye kikao kilichoandaliwa mapema Jumatano, jumla ya Maseneta 18 wametia saini ya kuidhinisha kuondolewa kwa Malala kutoka kwa wadhifa huo.

Siku ya Jumanne, Kiongozi wa wachache katika Seneti James Orengo, aliye pia Seneta wa Kaunti ya Siaya, aliitisha kikao hicho cha kumbandua Malala kutoka kwa wadhifa wa naibu wake.

Also Read
Wafugaji watakiwa kutumia mbinu za kisasa za ufugaji

Maseneta hao baadaye walimteua Seneta wa Kaunti ya Kilifi Stewart Madzayo kuwa Naibu mpya wa kiongozi wa wachache katika Seneti.

Maseneta hao wamehoji kwamba uamuzi wa kumteua Madzayo katika wadhifa huo umetokana na kwamba viongozi wengi wa Kaunti ya Kilifi walichaguliwa kwa chama cha ODM, hivyo wanapaswa kutuzwa.

Also Read
Isaac Mwaura atimuliwa rasmi Seneti

Kuanzia kwa Gavana, Seneta, Mwakilishi wa Wanawake, wabunge wote na wawakilishi wadi wengi katika kaunti hiyo walichaguliwa kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.

Seneta Malala, ambaye ni mfuasi wa Kinara wa ANC Musalia Mudavadi, anashtumiwa kwa kutofautiana wazi na chama cha ODM kwenye uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Matungu ambapo alimuunga mkono mgombea wa ANC Peter Nabulindo.

Also Read
Zaidi ya watoto 400 kaunti ya Garissa wanufaika na mpango wa wanaougua Kisukari

Aidha, anasemekana kutowahishimu baadhi ya vinara wa NASA na Naibu Kinara wa chama cha ODM Gavana Wyclif Oparanya, mbali na madai ya kutohudhuria vikao vya bunge hilo mara kwa mara.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi