Malkia Striker wapoteza mechi ya tatu mtawalia dhidi ya mabingwa wa dunia Serbia katika Olimpiki

Timu ya  Kenya ya Voliboli kwa akina dada imepoteza mchuano wa tatu mtawalia,  baada ya kupigwa na mabingwa wa dunia Serbia seti 3-0  katika pambano la  kundi A mapema Alhamisi  katika ukumbi wa Ariake mjini Tokyo Japan.

Also Read
Mashabiki wapigwa marufuku Olimpiki

Kenya walianza vyema mechi hiyo huku wakipoteza alama 21-25 kabla  ya kudoda katika seti ya pili wakishindwa alama 11-25 na  kuimarisha mchezo katika seti ya mwisho wakipoteza 20-25.

Also Read
Stars yaiangusha Sudan Kusini
Nahodha wa Kenya Mercy Moim akiokoa shambulizi

Ilikuwa mechi ya tatu mtawalia kwa Kenya kupoteza baada ya kushindwa na Japan na Korea Kusini seti 3-0 kila moja .

Sharon Chepchumba kwa mara nyingine tena ameiibuka mfungaji bora wa Kenya akizoa alama 12.

Also Read
CHAN kuingia siku ya 4 mjini Limbe Tanzania wakifungua pazia na Zambia

Malkia Strikers watarejea uwanjani  Jumamosi kwa mchuano wa nne dhidi ya Dominican Republic kabla ya kufunga kazi Agosti 2 dhidi ya Brazil.

  

Latest posts

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Gatlin na Omanyala tayari kuonyesha ubora wao Kip Keino Classic Jumamosi

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi