Malkia Strikers wajizatiti lakini waanguka seti 3-0 mikononi mwa wenyeji Japan

Timu ya taifa ya Kenya  ya Voliboli kwa akina dada,Malkia Striker  imejikakamua Jumapili adhuhuri  lakini ikashindwa na wenyeji Japan seti 3-0 katika mechi ya ufunguzi  ya kundi A ya  michezo ya Olimpiki iliyosakatwa katika ukumbi wa Ariake mjini Tokyo Japan.

Also Read
#KisaChangu: Dr Mukhisa Kituyi kuwania urais ili kukamilisha safari ya ukombozi

Malkia chini ya ukufunzi wa kocha Paul Bitok  ilianza vyema pambano hilo  lakini wakapoteza alama 15-25  na 11-25 katika seti ya pili.

Kenya iliimarisha mchezo katika seti ya tatu wakiongoza alama 23-20 lakini wakakosa kumakinika na kuwarusu Japan kutoka nyuma na kushinda pointi  25-23.

Also Read
Obiri kushiriki mita 5000 na 10000 michezo ya Olimpiki akiwinda dhahabu telezi

Sharon Chepcumba aliipatia Kenya pointi nyingi zikiwa 18.

 Malkia watarejea uwanjani Jumanne  dhidi ya  Korea Kusini katika mechi ya pili .

Also Read
Origi ajitolea kuwazima Comoros

Kenya inashiriki michezo ya Olimpiki kwa mara ya tatu baada ya kushiriki makala ya mwaka 2000 na 2004 ingawa hajawahinyakua hata seti moja.

 

 

 

 

 

  

Latest posts

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

NCIC kuwatumia vijana kuwa mabalozi wa amani kabla ya msimu wa uchaguzi

Tom Mathinji

Tusker ,Gor Mahia kufungua pazia kwa mechi ya Super Cup Jumatano

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi